Nani kamuua mchekeshaji maarufu nchini Tanzania, Emmanuel Mathias, maarufu MC Pilipili pengine ndio swali linalogonga vichwa vya wengi kwa sasa.
Nani amehusika kwenye mauaji yake na kwa nini amefikia hatua hiyo. Swali hilo linatokana na taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma kuthibitisha kwamba, kifo cha MC Pilipili kimetokana na kupigwa.
leo Novemba 18,2025 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gallus Hyela amesema kuwa, wameshirikiana na madaktari kuufanyia uchunguzi mwili wa MC Pilipili na kubaini kuwa kifo chake hakikuwa cha kawaida, hivyo wameanza uchunguzi mara moja kubaini waliohusika.
Chanzo; Mwananchi