Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Wanafunzi Wapigwa Shoti Darasani Arusha

Shule ya Msingi Naurei, iliyopo Kata ya Sokoni 2 Wilayani Arumeru Mkoani Arusha imekumbwa na tukio la kusikitisha baada ya nguzo ya umeme kupasuka na kuanguka karibu na Darasa upande wa madirisha wakati Wanafunzi wakiwa darasani na kusababisha mshtuko wa umeme (shoti) uliowaumiza baadhi ya Wanafunzi.

Baadhi ya Wanafunzi walipata majeraha sehemu mbalimbali za miili yao ikiwa ni pamoja na miguu na mapaja kufuatia taharuki hiyo ambapo Walimu na majirani walichukua hatua za haraka kuwaokoa Watoto na kuhakikisha walioumia wanapatiwa huduma na kupelekwa hospitali kwa matibabu.

Mtoto mmoja aliyepata majeraha makubwa alieleza jinsi alivyohisi mshtuko wa ghafla uliomwacha akiwa amechanganyikiwa ambapo alisema alihisi maumivu makali kwenye paja na mguu.

Aidha Wakazi wa eneo hilo pamoja na Wazazi wamesikitishwa na tukio hili wakisisitiza kuwa Mamlaka husika zichukue hatua za haraka kukagua na kutengeneza miundombinu ya umeme karibu na Shule ili kuzuia ajali kama hii kutokea tena.

 

Chazo: Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: