Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Rais Samia Awapa Pole Mabalozi Kuzimiwa Intaneti

Rais Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa mwaka 2025 Tanzania ilifanya Uchaguzi Mkuu wa saba kwa mafanikio, uliotoa matokeo chanya ikiwemo kuongezeka kwa uwakilishi wa wanawake bungeni hadi kufikia asilimia 44.

Hata hivyo, Rais Samia amekiri kuwepo kwa changamoto zilizojitokeza katika mchakato huo, hususan suala la kuzimwa kwa intaneti na kusitishwa kwa huduma za mtandao, na kutoa pole kwa mabalozi pamoja na wageni waliokumbwa na usumbufu uliotokana na hali hiyo, akiahidi kuwa Serikali imechukua hatua kuhakikisha tukio kama hilo halijirudii.

Rais Samia ameyasema hayo wakati akizungumza na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania, Ikulu, Chamwino jijini Dodoma na kueleza kuwa serikali imedhamiria kulinda usalama wao na kuhakikisha huduma muhimu zinapatikana bila vikwazo visivyo vya lazima.

Rais Samia pia amesema Serikali inatambua kwa uzito matukio yaliyojitokeza wakati wa siku ya uchaguzi na kipindi kilichofuata, akieleza kuwa hatua za kuingilia kati zilichukuliwa kwa lengo la kulinda amani na usalama wa nchi kwa mujibu wa Katiba.

Amehitimisha kwa kusema kuwa demokrasia ni mchakato unaokua taratibu na safari yake huambatana na changamoto mbalimbali, akibainisha kuwa hakuna mfumo mmoja wa kimataifa unaotoa suluhisho la changamoto hizo kwa kila nchi.

 

 

 

Chanzo; Global Publishers

Kuhusiana na mada hii: