Familia ya watu watatu, akiwemo baba, mama, na mtoto wa miaka mitatu katika Kata ya Kagera, Manispaa ya Kigoma Ujiji, wamefariki dunia baada ya nyumba yao kuchomwa moto mara baada ya kumwagiwa petroli usiku wa kuamkia Januari 25, 2026.
Chanzo cha tukio hilo la kinyama kinadaiwa kuwa ni mgogoro wa mirathi unaohusisha ugomvi wa mali za wazazi ndani ya familia hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma, Dkt. Rashid Chuachua, amethibitisha kutokea kwa mkasa huo akiwa katika eneo la tukio, ambapo ameeleza kuwa watu hao walikutwa wamefariki dunia baada ya nyumba yao kuteketea kabisa.
Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ili kubaini waliohusika na shambulio hilo la kikatili.
Chanzo; Mwananchi