Familia ya kijana Elia Msuya aliyefariki akiwa anapatiwa matibabu baada ya kudaiwa kupigwa jiwe kisogoni na mwenzake wakiwa kwenye ugomvi ambaye alikuwa ni mkazi wa kata ya Murieti Mkoani Arusha imeamua kuvunja sehemu ya nyumba yake ili azikwe baada ya kutokea kwa ugomvi ambao inaelezwa kuwa ndugu walitaka kuuza eneo hilo
Israeli Msuya msemaji wa familia hiyo amesema kwamba eneo hilo ni dogo na baadhi ya ndugu walitaka liuzwe ili wakalipe gharama za hospitali lakini kama familia wamekaa na kukubaliana kuwa eneo hilo halitauzwa bali litaachwa ili mke na watoto wa marehemu waishi hapo
Kwa upande wa dada wa marehemu ameomba serikali iweze kuwasaidia deni la shilingi million moja na laki tano wanalodaiwa hospitalini kwa kuwa familia haina uwezo
Chanzo; Millard Ayo