Mwili wa Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo aliyefariki dunia Februari 19, 2026 utazikwa Jumamosi ya Februari 28, 2026 eneo la Kituo cha Hija Pugu kilichopo Wilaya ya llala, jijini Dar es Salaam.
Katika moja ya mahojiano aliyofanya Kadinali Pengo wakati wa uhai wake, aliwahi kuzungumza kuhusu suala la maziko yake
atakapoondoka duniani, akisema tayari ameandaa sehemu ya
kizikwa Pugu, Dar es Salaam na kwenda mbali zaidi akisema
pia kaburi lilishaandaliwa.
Kwa mujibu wa ratiba ya mazishi iliyotolewa na Jimbo Kuu la Dar es Salaam leo, inaonesha Februari 27 saa 3:00 asubuhi, mwili wake utawasili Kanisa Kuu la Mt Yosefu na baada ya shughuli zote saa 10:00 itafanyika misa takatifu itakayoambana na mkesha wa sala na maombolezo.
Taarifa imesema Februari 28, saa 12:00 asubuhi mwili wake utaondoka Kanisa Kuu la Mt Yosefu kuelekea Kituo cha Hija Pugu Dar es Salaam na baada ya kutoa heshima za mwisho, saa 4:00 asubuhi itafanyika misa ya mazishi.
Chanzo; Bongo 5