Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Wanaopiga Simu Zimamoto Waonywa

Waziri wa Mambo ya Ndani, Patrobas Katambi, ametoa onyo kwa watu wenye tabia ya kupiga simu ya dharura ya zimamoto kwa lengo la kujifurahisha.

Amesema tabia hiyo ikiachwa iendelee, itafika wakati wananchi wenye dharura watakuwa wanapiga simu lakini watoa huduma watadhani ni wale wanaopiga simu za uongo kwa lengo la kujifurahisha.

Pia amewataka watu wote wanaojenga majengo yao, kuhakikisha wanafanyiwa ukaguzi na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili kupunguza ajali za moto zinazoweza kuzuilika.

Waziri Katambi ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake katika Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, ziara aliyofanya kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuiongoza wizara hiyo.

 

 

Chanzo; Global Publishers

Katika ziara hiyo, aliambatana na Naibu Waziri, Ayoub Mohamed Mahmoud.

Kuhusiana na mada hii: