Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Kwa Tuhuma za Mauaji ya Mkewe Helakumi Asakwa

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamtafuta Helakumi Kacheri kwa tuhuma za mauaji ya mkewe.
Tukio hilo limetokea Januari 4, 2026 mchana eneo la Kitongoji cha Tindegela Kata ya Singisa Wilaya ya Morogoro wakati wawili hao wakiwa shambani.

Mtuhumiwa alimshambulia marehemu kwa silaha yenye makali sehemu mbalimbali za mwili wake akimtuhumu marehemu kuendeleza mahusiano ya karibu na mzazi mwenzake wa awali. Mtuhumiwa alitoroka baada ya kutekeleza mauaji hayo.

Wakati huohuo, Jeshi la Polisi Morogoro linafanya uchunguzi wa matukio mawili ya vifo katika Wilaya ya Kilombero na Mvomero. Tukio la awali limetokea Januari 4, 2026 asubuhi huko katika Kitongoji cha Isago Kata ya Mngeta Wilaya ya Morogoro ambapo Jese Melumba (49) mkulima na mkazi wa Isago alikufa akidhaniwa kunywa sumu ya kuulia magugu ya shambani.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwepo mabaki ya dawa ya kuulia magugu iitwayo Banafos.
Tukio lingine limetokea Januari 3, 2026 huko katika Kitongoji cha Doma stand Kijiji na Kata ya Doma ambapo Ally Charles Dagaza (38) mkulima na mkazi wa Doma alikufa akiwa shambani kwake baada ya kukanyagwa na mnyama Tembo wakati akiwa analinda miche ya nyanya na zao la pilipili.

Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi wenye taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa mtuhumiwa aliyetenda tukio mauaji aziwasilishe kituo cha Polisi kwa hatua zaidi za kisheria.

 

 

Chanzo; Bongo 5

Kuhusiana na mada hii: