Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

TEC Yahimiza Uchunguzi Huru Vurugu Oktoba 29

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), limekemea vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025, huku likitoa wito wa uchunguzi huru utakaoshirikisha wadau mbalimbali wakiwemo wa kidemokrasia ufanyike.

Mbali na hilo, TEC limetaka watu wote waliokamatwa kabla, wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi kuachiwa huru. Sambamba na hilo, baraza hilo, limekumbushia kuanza kwa mchakato wa Katiba Mpya.

Hata hivyo, jana Ijumaa Novemba 14, 2025 akizindua Bunge na kutoa mwelekeo wa Serikali kwa miaka mitano ijayo, Rais Samia Suluhu Hassan alilani matukio hayo, akisema tayari Serikali imechukua hatua ya kuunda Tume ya kuchunguza yaliyotokea ili kubaini kiini cha tatizo.

“Taarifa hiyo itatuongoza kujielekeza kwenye mazungumzo ya kuleta maelewano na amani,” amesema Rais Samia akiwa bungeni jijini Dodoma.

Leo Jumamosi Novemba 15, 2025 akisoma tafakuri ya pamoja ya Maaskofu wa Kanisa hilo, kufuatia tafakari na sala walizofanya kwa siku nne kuanzia Novemba 11 hadi 14, Rais wa baraza hilo, Askofu Askofu Wolfgang Pisa amesema kanisa linakemea yaliyotokea.

Kwa mujibu wa Askofu Pisa, maandamano hayo yaliyosababisha vurugu yaliyozaa mauaji, watu kujeruhiwa, uharibifu na upotevu wa mali binafsi na za umma, hali iliyowaumiza na kuwasononesha jamii ya Watanzania.

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: