Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

TMDA na Mpango wa Kulinda Afya ya Jamii, Wanaokiuka Ubora Kubanwa

Menejimenti ya Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA imekutana Mkoani Morogoro ili kujadili rasimu ya Mpango Mkakati Mpya wa Mamlaka wa miaka mitano, 2026/27-2030/31 unaoakisi utekelezaji wa Dira ya Taifa ya 2050.

Rasimu ya Mpango Mkakati huo ni ya Sita kufuatia kukamilika kwa ufanisi kwa Mpango Mkakati wa Tano. Mpango Mkakati wa Sita wa TMDA unatarajiwa kuanza kutumika mnamo tarehe 01, Julai, 2026.

Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Dkt. Adam Fimbo amesema, rasimu ya Mpango Mkakati husika inalenga katika kuhakikisha ubora, usalama na ufanisi wa bidhaa za dawa, vifaa tiba na vitendanishi kwa lengo la kulinda afya ya Jamii.

"Kuimarika kwa afya na ustawi wa Watanzania wote kupitia udhibiti bora unaokidhi viwango vya kitaifa ndio lengo letu, dhamira Mpya ya Taasisi itakuwa " Kulinda Afya ya Jamii kwa kuhakikisha, usalama, ubora na ufanisi wa dawa, vifaa tiba, vitendanishi na bidhaa zote zinazohusiana na afya", amesema Dkt Fimbo.

 

 

Chanzo; Clouds Media

Kuhusiana na mada hii: