Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania, Prof. Said A. Mohamed, ametangaza rasmi matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Kidato cha Nne (CSEE) 2025 leo tarehe 31 Januari, 2026 jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa matokeo hayo, jumla ya watahiniwa 526,620 kati ya 595,810 waliopata matokeo wamefaulu mtihani huo, hatua inayodhihirisha ongezeko la ufaulu kwa mwaka huu.
Wanafunzi 77 wamefutiwa matokeo ya kidato cha 4 kwa sababu za kuandika lugha chafu na wengine kwa udanganyifu katika mtihani kati ya hao 47 kutoka kwenye vituo vya mtihani na 30 kutoka shule.
Chanzo; Global Publishers