Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amelipongeza Jeshi la Polisi Visiwani Zanzibar kwa juhudi zake za kupambana na uhalifu, hali iliyosababisha kupungua kwa matukio 746.
Takwimu zinaonesha kuwa matukio 3,091 yaliripotiwa mwaka 2024, huku mwaka 2025 yakiripotiwa matukio 2,345.
Akizungumza na Uongozi wa Juu wa Jeshi la Polisi Visiwani humo, Waziri Katambi alizungumzia pia suala la ulinzi kwa watalii, akisisitiza jitihada zilizofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, katika kutangaza na kukuza sekta ya utalii.
Aidha, aligusia masuala ya mauaji yanayotokana na wananchi kujichukulia sheria mkononi pamoja na makosa ya barabarani yanayosababishwa na watumiaji wa vyombo vya moto kutofuata sheria za usalama barabarani.
Chanzo; Global Publishers