Jeshi la Polisi Dar es salaam limewadhibiti Wafuasi wa Chama cha CHADEMA huku baadhi yao wakiadhibiwa kwa kupigwa virungu na mateke baada ya kuibuka kwa hali ya taharuki katika viunga vya Mahakama Kuu ya Tanzania Masijala ndogo ya Dar es salaam.
Wafuasi hao walifika maeneo ya Mahakamani kwa ajili ya kufuatilia mwenendo wa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.
Chanzo: Millard Ayo