Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imefanikiwa kumnasa chui aliyekuwa akiishi katika makazi ya watu na kuhatarisha maisha yao pamoja na mifugo katika Kijiji cha Mwalali, wilayani Itilima, mkoani Simiyu.
Daktari wa wanyamapori kutoka TAWA, Elias Mwamsabe, amesema kuwa baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi, walifika kwa mara ya kwanza wakiwa na askari, lakini walibaini kuwa eneo ambalo chui huyo alikuwa akiishi halikuwa rahisi kumpata.
Wananchi wamepongeza hatua hiyo na kueleza kuwa chui huyo alikuwa tishio kwao.
Chanzo; Global Publishers