Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Chalamila Aibuka Kimara Kauli za Hatuitaki CCM Hazisaidii, Mabasi Yanakuja

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewataka wananchi kuwa watulivu kuhusu changamoto za usafiri wa mabasi ya mwendokasi, akisisitiza kuwa huduma mpya zinakuja huku akionya kuwa kuimba kauli za kupinga Chama cha Mapinduzi (CCM) hakutasaidia kutatua tatizo hilo.

Akizungumzamapema leo Jumatano, Oktoba 1, 2025, katika kituo cha Kimara Mwisho, Chalamila amesema tayari zaidi ya mabasi 200 mapya yameshapakiwa kuanza kazi, huku mengine 150 yakiwa mbioni kuanza kutoa huduma katika njia ya Mbagala.

“Wiki hii kabla haijaisha kutakuwa na mabasi mapya machache yatakayoingia wakati tunatafuta suluhu ya kudumu. Huyu mtoa huduma wa sasa tunamuondoa na tunaleta mtoa huduma mpya,” amesema Chalamila.
Aidha, amesisitiza kuwa malalamiko ya wananchi hayataondoa changamoto ya mabasi yaliyopo.

“Hata mkisema hamuitaki CCM, nimeona kwenye clip, haisaidii. Mwisho wa siku mnahitaji mabasi, na yakija lazima mpande. Tunahitaji busara ya wananchi na busara ya Serikali ili kupata suluhu ya kudumu,” ameogeza Chalamila.

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: