Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Watano Wafariki kwa Kufukiwa na Udongo Tanga

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limethibitisha kutokea kwa ajali ya kusikitisha iliyopelekea vifo vya watu watano baada ya kufukiwa na udongo wakati wakifanya shughuli za uchimbaji mchanga katika machimbo ya Bolbit, Kijiji cha Makuyuni, Wilaya ya Korogwe.

Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi, ajali hiyo imetokea leo Februari 15, 2026 majira ya saa 11:30 jioni, ambapo ngema ya udongo ilikatika na kuwafukia wachimbaji hao.

Jitihada za uokoaji zilizohusisha Jeshi la Polisi, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na wananchi zilifanikiwa kutoa miili ya marehemu watano, ambayo imehifadhiwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Korogwe Vijijini Makuyuni kwa taratibu zaidi.

Waliopoteza maisha ni Shabani Mrisho maarufu Mwantembo (31), Yusuph Abdalah maarufu Kibaya, Juma Hatibu maarufu Msikiti (49), Nurdini Amiri maarufu Daffa (30) na Zamiru Miraji maarufu Daffa (35), wote wakiwa wakulima na wakazi wa Makuyuni.

Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wananchi wanaojihusisha na shughuli za uchimbaji kuzingatia misingi ya usalama mahali pa kazi ili kuepusha majanga yanayoweza kusababisha madhara makubwa kwa familia na jamii.

Aidha, viongozi wa vijiji na mitaa wamehimizwa kusimamia shughuli za machimbo kwa karibu ili kuhakikisha zinafanyika katika mazingira salama.

Taarifa hii imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga.

 

 

Chanzo; Global Publishers

Kuhusiana na mada hii: