Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Wezi Waingia Kuiba Msibani, Wasahau Simu

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, familia ya Daniel Peter Wakazi wa Kata Malangarini, Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha inayoomboleza msiba wa Ndugu yao, imejikuta ikipata maumivu juu ya maumivu baada ya Wezi kuingia ndani ya nyumba yao kwa kupita kwenye paa na kuiba vitu mbalimbali ikiwemo pikipiki na simu baada ya Wafiwa kupatwa na usingizi mzito.

Edna Samson mmoja wa Wanafamilia hao, amesema siku ya tukio walilala saa tisa usiku ambapo baada ya kulala walipitiwa na usingizi mzito ambao ulifanya wasisikie chochote kikiibwa ambapo ameongeza kuwa waliporipoti tukio hilo Polisi na Watuhumiwa kupatikana lakini baadae wakaachiwa.

Edna na Familia yake wameziomba Mamlaka ziendelee na uchunguzi zaidi na hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi ya Wahusika wote, juhudi za AyoTV kupata taarifa kuhusu wizi huu kutoka kwa Kamanda wa Polisi Arusha bado zinaendelea.

 

 

Chanzo; Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: