Fundi ujenzi na mkazi wa kata ya Lukobe manispaa ya Morogoro Stanley Richard Kunambi anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa tuhuma na kuzini na maharamu wake.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mama amesema tukio hilo limeripotiwa Septemba mmsi mwaka huu kwa nyakati tofauti mtuhumiwa alifanya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa mtoto wake wa kumzaa wa miaka kumi na tatu.
Kamanda Mkama amesema kitendo hicho cha kumuingilia kinyume na maumbile kimemsababishia maumivu makali na upeleleze unafanyika kwa ajili ya hatua za kisheria.
Mmoja wa wakazi wa manispaa ya Morogoro Liberata Mugalula amelaani kitendo cha baba kumlawiti binti yake huku akitoa ushauri kwa wanawake wanapotengana na wenza wao kukaa na watoto wao badala ya kuwaacha kwa wazazi wa kiume kwani usalama wa watoto unakuwa Mdogo.
Pis kamanda Mkama ameaelezea mafanikio waliyoyapata katika jeshi la polisi mkoa wa Morogoro katika kukabiliana na vitendo vya uhalifu.