Wakili Boniface Mwabukusi, Rais wa Chama cha Wanasheria cha Tanganyika “TLS” ameoridhesha hoja za msingi walizowasilisha kwa Rais wa Jamhuri wa Tanzania, kupitia kipindi cha 360 cha Clouds Tv.
"Hoja za msingi tulizozungumza na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan ni suala la sheria na kanuni za tume za uchaguzi kwanini zinalalamikiwa na maeneo yanayolalamikiwa.
"Na jambo la pili tulilowasilisha kwake ni suala la umuhimu wa kuwepo kwa mazungumzo au mjadala wa Kitaifa kabla na baada ya uchaguzi ili kulileta Taifa pamoja. Na sisi kuona namna gani tunapita kwenye hii changamoto salama.
"Na jambo la Tatu ni shauri la Mhe. Tundu Lissu linaloendelea mahakamani na mtazamo wetu kidemokrasia na Kimataifa kwa Taifa letu na kuomba waone kitu gani kama Serikali watafanya. Na kwamba shauri la Tundu Lissu watu wanaliangalia kwa sura tofauti na halileti taswira nzuri kwa Taifa letu"- Mwabukusi
Chanzo: Clouds Tv