Hawa ni wananchi wa kijiji cha Kanioga kata ya Lugelele wilaya ya Mbarali hapa mkoani Mbeya, wakieleza adha wanazozipitia wakati wa kufuata huduma za kijamii mji wa Rujewa kutokana na kukosa daraja kwenye mto Mbarali unaoziunganisha kata hizo.
Wananchi hao wamesema kwa kipindi kirefu wamekua wakilazimika kupiga mbizi ili kuvuka mto huo nakufika upande wa pili jambo ambalo limekua likighalimu maisha yao.
Diwani wa kata ya Lugelele anasema pamoja na wananchi wake kukosa huduma za kijamii kwa wakati kupitia mto huo, vifo kwa wananchi na watoto imekua ni sehemu ya maisha yao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbarali Raymond Mweli anaeleza mipango ya halmashauri hiyo ilikuwanusuru wananchi hao ikiwa ni pamoja na kutenga fedha zaidi ya millioni 900 zitakazo saidia kuboresha miundombinu.
Chanzo; Wasafi Media