Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limemtia nguvuni Marwan Said (24), mkazi wa Kariakoo Wilaya ya Ilala Dar es Salaam kwa tuhuma za kujaribu kuua baada ya kumjeruhi vibaya kwa kumkata na kitu chenye ncha kali kwenye kiganja cha mkono Nurdin Yahaya (29), dereva pikipiki na mkazi Mbezi.
Tukio hilo limetokea leo Februari 2,2026 saa 05:40 asubuhi katika Mtaa wa Pemba na Bonde Kariakoo. Na kwamba chanzo cha tukio hilo ni madai ya majeruhi kumdai mtuhumiwa Sh. 10,000 kama malipo ya mzigo aliotumwa kutoka Sinza.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Jumanne Muliro, majeruhi yuko hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu na Mtuhumiwa atafikishwa kwenye mamlaka zingine za kisheria haraka iwezekanavyo.
Chanzo; Eatv