Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mtoto wa Miaka 16 Atoweka Nyumbani, Wzazi Wadai Alielekea Shule

Mtoto Bryson Gift Daima (16), mkazi wa Mtaa wa Sawe, wilayani Babati mkoani Manyara, ameripotiwa kutoweka nyumbani kwao ambako alikuwa akiishi na wazazi wake.

Baba mzazi wa mtoto huyo Gift Daima amesema mwanawe aliondoka nyumbani tarehe 2 Mei, 2024, akielekea shuleni kama ilivyokuwa kawaida, lakini hakurejea tena nyumbani hadi sasa.

Amesema baada ya jitihada za kumtafuta bila mafanikio, familia ilifanikiwa kukuta nguo za shule pamoja na madaftari ya mtoto huyo katika nyumba moja ambayo haijakamilika, iliyopo mtaani hapo.

Aidha, wazazi wamesema kabla ya kutoweka, mtoto huyo alikuwa ameagizwa na uongozi wa shule afike shuleni akiwa na mzazi, lakini hakuwahi kuwataarifu wazazi wake kuhusu agizo hilo.

Hata hivyo, familia imeripoti tukio hilo katika kituo cha polisi, na kwamba Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara linaendelea na juhudi za kumtafuta mtoto huyo.

 

 

Chanzo; Wasafi

Kuhusiana na mada hii: