Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Kanisa Katoriki Mbeya Kuwaombea Waliofariki Oktoba 29

Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mbeya limetangaza nia maalumu ya kuwaombea watu waliopoteza maisha au kujeruhiwa wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025.

Siku hiyo, shughuli ya upigaji kura kuwachagua Rais, wabunge na madiwani, ililoambatana na maandamano na vurugu katika baadhi ya maeneo nchini zilizopelekea watu ambao idadi yao haijafahamika kuuawa, kujeruhiwa na wengine hawajulikani walipo.

Hata waliosalimika walilazimika kujifungia ndani kwa takribani siku sita huku shughuli za kijamii zikisimama.

Katika mujibu wa taarifa iliyotolewa Novemba 4, 2025 kupitia kwa katibu wa kanisa hilo, Padri Henry Mwalyenga, parokia zote za jimbo kuu zinaagizwa kuwa na nia maalumu ya kuwaombea marehemu na majeruhi.

Maombi hayo yanatarajia kufanyika Novemba 9, 2025 ambayo ni Dominika ya 32 ya mwaka C, ambapo siku hiyo alasiri, kutakuwa na misa maalumu ya kijimbo kwa ajili ya kuwaombea waathirika hao katika Kanisa la Hija Mwanjelwa jijini Mbeya.

Akizungumza kwa njia ya simu, Askofu Mkuu wa Jimbo hilo, Gervas Nyaisonga amethibitisha kuwepo maombi hayo, akieleza lengo ni kuliombea Taifa na wale waliopata madhila wakati na baada ya uchaguzi.

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: