Hatima ya uhalali wa maombi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu kujumuishwa katika kesi ya madai ya mgawanyo usio sawa wa itaamuliwa Machi 3, 2026.
Kesi hiyo ya madai namba 8323 ya mwaka 2025 imefunguliwa na Makamu Mwenyekiti mstaafu wa Chadema, Said Issa Mohamed, na wajumbe wawili wa Bodi ya Wadhamini wa Chadema kutoka Zanzibar, Ahmed Rashid Khamis na Maulida Anna Komu.
Wadaiwa katika kesi hiyo inayosikilizwa na Jaji Hamidu Mwanga, Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam ni Bodi ya Wadhamini Waliosajiliwa wa Chadema na Katibu Mkuu wa chama hicho.
Lissu aliwawasilisha maombi, akiomba kuunganishwa kwenye kesi hiyo kama mdaawa mwenye maslahi. Wajibu maombi katika shauri hilo ni pamoja na wadai katika kesi ya msingi yaani Said na wenzake kwa upande mmoja na Wadhamini wa Chadema na Katibu Mkuu ambao ni wadaiwa katika kesi ya msingi.
Hata hivyo, wajibu maombi hayo ambao ni wadai katika kesi ya msingi, ya ni Said na wenzake wamemuwekea pingamizi la awali ambalo limesikilizwa leo Jumanne Februari 17, 2026, ambapo pande zote zimetoa hoja zake kutetea msimamo wake, ambapo mahakama imepanga kutoa uamuzi Machi 3, 2026.
Chanzo; Mwananchi