Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Waandishi Wapigwa Msasa Kuhusu Mabusha

Wizara ya Afya Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Idara ya Afya, imeendesha mafunzo maalumu kwa waandishi wa habari kuhusu magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, yakiwemo ugonjwa wa matende na mabusha/ngirimaji.

Mafunzo hayo yaliyowakutanisha Maafisa Habari pamoja na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari yamelenga kuwajengea uwezo wa kutoa taarifa sahihi kwa jamii, pamoja na kuhamasisha wananchi kuhusu uwepo wa kambi ya upasuaji wa mabusha katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi Sokoine, iliyoanza kutoa huduma kuanzia Februari 09 na inatarajiwa kukamilika Machi 05, 2026, ambapo wagonjwa takribani 500 wanatarajiwa kufikiwa.

Akizungumza katika semina hiyo, Dkt. Golinja Anthony kutoka Wizara ya Afya amesema mafunzo hayo yanawalenga wanahabari kama wadau muhimu wa kufikisha ujumbe kwa jamii kuhusu namna magonjwa hayo yanavyoenea, njia za kujikinga pamoja na matibabu yake, ili kuondoa dhana potofu zilizojengeka miongoni mwa wananchi.

Ameeleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za Serikali kuboresha huduma za afya na kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele, huku wananchi wakihimizwa kujitokeza kwa wingi katika vituo vilivyoainishwa kwa ajili ya uchunguzi na matibabu mapema.

 

 

Chanzo; Global Publlishers

Kuhusiana na mada hii: