Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Regina Ndege Qwaray amesema ajira za utumishi hupatikana kwa ushindani na uwazi na kwamba Vijana wanaojitolea kazini (field) huwezeshwa kupata ujuzi na uzoefu na uwezo wa kushindana pindi ajira zinapotoka lakini sio kwamba Vijana wenye uzoefu wanapaswa kupewa kipaumbele kuliko wengine kwakuwa wapo Vijana waliopewa nafasi za kujitolea kwa kupendelewa tu makazini.
Naibu Waziri amesema hayo Bungeni Jijini Dodoma leo February 04,2026 wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Vijana, Latifa Khamis Juwakali aliyehoji “Je, Serikali haioni haja ya kuwapa kipaumbele cha ajira Vijana watakaofanya vizuri wakiwa field hasa kwenye miradi ya Serikali?”
Naibu Waziri Regina amesema “Kwa mujibu wa sera ya Menejimenti na ajira katika Utumishi wa Umma toleo la pili la mwaka 2008 ikisomwa pamoja na sheria ya Utumishi wa Umma sura 298, ajira katika utumishi wa umma hupatikana kwa ushindani na uwazi, kujitolea huwezesha Vijana kujipatia ujuzi wa ziada na kuwapa uzoefu na uwezo wa kushindana pindi ajira zinapotangazwa”
“Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa Vijana kupata mafunzo kwa vitendo ili kujipatia sifa za ajira katika utumishi wa umma pindi nafasi za taaluma zao zinapotangazwa na Serikali”
Chanzo; Millard Ayo