Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Shahidi Adai Hotuba ya Lissu Ilimshawishi Kuvuruga Uchaguzi

Shahidi wa tano wa Jamhuri katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, ameieleza Mahakama kuwa aliposikiliza hotuba ya Lissu kuhusu kukinukisha kuzuia uchaguzi kwa kuuvuruga alishawishika kuwa miongoni mwa vijana watakaoshiriki mpango huo.

Shahidi huyo ambaye ni miongoni mwa mashahidi fiche wa Jamhuri (waliopewa ulinzi, yaani wasiotakiwa kuonekana wala kutambulika), ametambulishwa kwa jina la P6 (24) na ametoa ushahidi wake akiwa ndani ya kizimba maalumu ambacho hakimuwezeshi kuonekana kwa wasikilizaji wala mshtakiwa isipokuwa kwa majaji tu.

Lissu anakabiliwa na shtaka moja la uhaini kinyume na kifungu cha 39(2) (d) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, linalotokana na maneno aliyoyatamka kuhusiana na kusudio la kuzuia kufanyika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Kesi hiyo inayosikilizwa Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam na jopo la majaji watatu linaloongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Iringa, Dunstan Ndunguru akishirikiana na James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde, iko katika hatua ya usikilizwaji wa ushahidi wa upande wa mashtaka.

Katika mwendelezo wa ushahidi wa Jamhuri, shahidi huyo wa nne katika ushahidi wake leo Alhamis, Februari 13, 2026 akiongozwa na mwendesha mashtaka, Wakili wa Serikali, Cuthbert Mbilingi, ameeleza kuwa, yeye ni mkazi wa Songea na ni ofisa usafirishaji kwa kutumia bodaboda.

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: