Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Miili Miiwili Yabaki Mochwari, Ajali ya Maseyu

Serikali mkoani Morogoro imeongeza muda wa utambuzi wa miili ya marehemu waliopata ajali ya magari mawili kugongana uso kwa uso na kuteketea kwa moto kwenye eneo la Maseyu mkoani Morogoro kutokana na miili miwili kati ya 10 kuendelea kubaki kwa siku 16 sasa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwenye hospitali ya Rufaa (MRRH).

Kwa Mujibu wa Kaimu Ofisa Mahusiano wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Morogoro Scolastica Ndunga amesema serikali ya mkoa imeamua kuongeza muda kutokana na kuwa miili hiyo kuwa tayari imeshapitisha siku 14 ambazo zimewekwa kitaalamu kwa ajili ya miili yoyote kuzikwa na serikali, ili kusaidia ndugu kujitokeza kwa utambuzi wa miili ikiwa ni pamoja na kupimwa vinasaba (DNA) na kuruhusiwa kwenda kuzika.

"Ni kweli leo ni siku ya 16 tangu ajali hiyo itokee lakini miili miwili bado haijatambuliwa wala ndugu hawajajitokeza kutambua na tayari miili 8 imeshatambuliwa na kwenda kusitiriwa na ndugu zao baada ya kupima vinasaba, miili miwili iliyobaki ni ya jinsia ya kiume na Mkuu wa mkoa wa Morogoro Adam Malima ametoa agizo kuwa siku ziongezwe kwa ajili ya utambuzi wa miili hiyo". Amesema Scolastica.

Akizungumzia hali za majeruhi Scolastica amesema majeruhi mmoja anayejulikana kwa jina la Hadija Suleiman (23) kati ya majeruhi 23 wa ajali hiyo amebaki akipatiwa matibabu kwenye hospitali hiyo na kwamba anaendelea vizuri ambapo tayari ameshafanyiwa upasuaji wa mifupa kwa mara ya pili.

Ajali hiyo ilitokea Desemba 31 mwaka jana majira ya usiku katika kijiji cha Maseyu Kata ya Gwata mkoani Morogoro.

 

 

 

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: