Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Shahidi wa 9 Kesi ya Dkt. Manguruwe na Milioni 20 Yake

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeendelea kusikiliza ushahidi wa kesi ya utakatishaji fedha na biashara ya upatu inayomkabili Mkurugenzi wa kampuni ya Vanilla International Limited, Simon Mkondya (Dk. Manguruwe), na mwenzake Rweymamu John.

Shahidi wa tisa, Abeid Shekimweri, ameieleza mahakama jinsi alivyopoteza jumla ya shilingi milioni 20 baada ya kushawishika na matangazo ya vyombo vya habari kuwekeza katika zao la vanilla na yangiyangi akiahidiwa kupata faida ya zaidi ya shilingi milioni 120 ndani ya mwaka mmoja na nusu.

Shahidi huyo amebainisha kuwa baada ya kuwekeza fedha hizo, alipewa maelezo kuwa mashamba yake yapo Bungi, Zanzibar, lakini alipokwenda kufanya ukaguzi alikuta hakuna shamba lolote.

Amesema jitihada zake za kufuatilia haki yake ziligonga mwamba baada ya wahusika kumtaka atulie, hadi alipoona taarifa za kukamatwa kwa washtakiwa hao kwenye vyombo vya habari na kuamua kutoa maelezo polisi kisha kufika Mahakamani kutoa ushahidi.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na jumla ya mashtaka 28, yakiwemo ya kujipatia zaidi ya shilingi milioni 90 kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa watu 19 tofauti kati ya mwaka 2020 na 2023.

Aidha, Dk. Manguruwe anatuhumiwa kutumia fedha hizo za upatu kununua viwanja tisa katika eneo la Idunda mkoani Njombe, jambo ambalo ni kosa la kisheria la kutakatisha fedha zinazotokana na makosa ya jinai.

 

 

Chanzo; Itv

Kuhusiana na mada hii: