Serikali ya Tanzania imesajili rasmi dawa ya Lenacapavir kwa ajili ya kudhibiti na kuzuia maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU), hatua inayotajwa kuleta mapinduzi katika tiba na kinga dhidi ya maambukizi hayo nchini.
Dawa hiyo ya sindano inayozuia maambukizi ya VVU, yenye uwezo wa kutumika kama mbadala wa ARV’s kwa wenye maambukizi ya VVU, ilionesha ufanisi kwa asilimia 100 katika jaribio la kwanza la utafiti Uganda mwaka 2025.
Tayari mchakato wa kuipitia dawa hiyo na kuiingiza kwenye mwongozo wa kitaifa wa matibabu kama miongoni mwa dawa zitakazotumika katika kudhibiti VVU, umekamilika.
Akizungumza jana Jumanne, Februari 24, 2026 Mfamasia Mkuu wa Serikali, Daud Msasi amesema dawa hiyo tayari imetambuliwa na kusajiliwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), huku mchakato wa kuiingiza rasmi kwenye matumizi ya kitaifa ukiendelea kupitia mapitio ya miongozo ya matibabu.
Chanzo; Mwananchi