Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mpina Agoma Kutoa Ushahidi kwa Tume

Mwanachama Mwandamizi wa Chama cha ACT Wazalendo, Luhaga Mpina, amekataa kushirikiana na Tume ya Rais ya kuchunguza matukio ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, akisisitiza kuwa hatatoa ushirikiano wowote kwa chombo hicho.

Katika barua yake iliyotumwa kwa Katibu wa Tume hiyo, Onorius Njole, imedai Mpina ameeleza kwamba hatahudhuria kikao kilichopangwa kufanyika leo katika Ukumbi wa Manyara, Benki Kuu, Jijini Dar es Salaam.

Mpina amebainisha kwamba uamuzi wake unatokana na msimamo rasmi wa chama cha ACT Wazalendo uliotolewa Novemba 18, 2025, ambao unapinga na kukataa kuundwa kwa tume hiyo.

Chama hicho kimesema hakitashiriki kwa namna yoyote katika uchunguzi huo, kwa sababu kinaitambua tume hiyo kama 'chombo kisicho huru'.

Mpina amekumbusha msimamo wake wa Disemba 6, 2025, akisisitiza kuwa tume hiyo haikufuata taratibu za Kimataifa za usuluhishi wa migogoro na hivyo haina sifa za kufanya uchunguzi wa haki na usawa, 'Hatutatoa ushahidi wala kutoa ushirikiano wowote' Amesema Mpina.

 

 

Chanzo; Itv

Kuhusiana na mada hii: