Watu wawili wamenusurika kifo baada ya kutokea ajali ya moto katika Jengo la NSSF lililopo mtaa wa Azikiwe na Samora, eneo la Posta jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, sehemu kubwa ya jengo pamoja na mali zilizokuwemo zimefanikiwa kuokolewa, kufuatia juhudi za haraka za vikosi vya zimamoto vilivyowasili eneo la tukio.
Jeshi hilo limeeleza kuwa chanzo cha moto huo bado hakijafahamika, huku uchunguzi ukiendelea ili kubaini chanzo na kiwango cha uharibifu uliosababishwa na tukio hilo.
Chanzo; Global Publishers