Mahakama Kuu ya Zanzibar imemuhukumu Mwanamke Mmoja Aliyefahamika kwa jina la Khadija Shabani Ali (35) mkazi wa Chukwani, Unguja kifungo cha Miaka 20 jela (Chuo cha Mafunzo) mara baada ya kukutwa na hatia ya kujaribu kuua kinyme cha Sheria
Khadija amehukumiwa kutumikia kifungo hicho kwa kutenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 193(b) cha Sheria namba 6/2018 ambapo inaelezwa kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo febriari 9, 2025 ambapo alimchoma Maymuna Said Suleiman ambae ni Mke mwenzie kisu kwenye paji la uso, shingoni, nyuma ya bega na kwenye vidole vya mikono.
Aidha Akisoma maelezo ya Hukumu Jaji wa Mahkama Kuu ya Zanzibar, Aziza Iddi Suwedi amesema Mahakama imejiridhisha na Ushahidi uliotolewa Mahakamani na kumtia hatiani mshtakiwa kwa kosa hilo ambapo jumla ya mashahidi kumi (10) walitoa Ushahidi wao Mahakamani.
Chanzo' Millard Ayo