Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa , ameeleza kuwa Tanzania ina mpango wa kuanza kuzalisha dawa za ARVs (Antiretroviral Drugs) nchini ili kupunguza utegemezi wa dawa hizi kutoka nje.
Kauli hiyo alitoa wakati wa ziara ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ya afya inayotekelezwa na serikali ya awamu ya sita.
Mchengerwa alisema kuwa ni muhimu kwa taifa kuzalisha dawa zake mwenyewe ili kuwa na uhakika wa upatikanaji wa dawa bila kutegemea nje, na kwamba lengo ni kufikia asilimia mia moja katika uzalishaji wa dawa hizo.
Waziri Mchengerwa amesema hatua hii ni muhimu si tu kwa kuboresha huduma za afya nchini, bali pia kwa kuongeza uwezo wa nchi katika sekta ya afya na kupunguza gharama za ununuzi wa dawa kutoka nje.
Chanzo; Crown Media