Wakati kesi ya madai inayokikabili chama cha Demokrasia na Maendeleo ikiendelea mahakamani, Mwenyekiti wa Chama hicho, Tundu Lissu amewasilisha maombi katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam akiomba kujumuishwa kama mdaiwa katika kesi ya Mgawanyo wa Mali inayokikabili chama chake.
Maombi hayo yaliwasilishaa Novemba 10, 2025 na tayari taratibu zote za kimahakama zimefanyika ikiwemo kuwasilisha maombi hayo katika mfumo wa mahakama pamoja na kulipia. Hivyo kwa sasa kilichobaki ni Mahakama kuyapangia tarehe maombi hayo ili yaweze kusikilizwa.
Mkurugenzi wa Sheria wa CHADEMA, Wakili Gaston Garubindi amekiri kuwa ni kweli maombi yameshasawasilishwa na yamelipiwa ada kinachosubiriwa ni ofisi ya Jaji Mwanga kutokana na kalenda ya mahakama na utapangwa utaratibu rasmi wa kutoa wito na maombi kusikilizwa.
Katika shauri hilo la msingi la madai lenye namba 8323/2025 wadaiwa ni Bodi ya Wadhamini wa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, hivyo maombi ya Lissu yakikubaliwa atakuwa mdaiwa wa tatu.
Shauri hilo limefunguliwa na Said Issa Mohammed na wenzake wakidai kuwepo kwa upendeleo kwenye ugawaji wa rasilimali za chama, upande wa bara ukipendelewa zaidi kuliko Zanzibar.
Chanzo; Eatv