Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Tume ya Uchunguzi Matukio Oktoba 29 Yaongezewa Siku 42

Tume ya kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 imeongezewa siku 42 kuanzia Ijumaa, Februari 20, 2026. Tume hiyo iliyoteuliwa na kuzinduliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, ilipewa siku 90 kukamilisha kazi yake, na kuanzia Novemba 20, 2025, siku hizo zilikamilika Februari 20, 2026.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na tume hiyo, nyongeza ya siku 42 imefikiwa ili kuipa muda tume hiyo kukamilisha uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025. Kwa nyongeza hiyo ya muda, tume sasa inapaswa kukamilisha kazi na kuwasilisha taarifa yake kabla au ifikapo Aprili 3, 2026.

Miongoni mwa matukio yaliyotokea katika mikoa mbalimbali nchini ni maandamano yaliyozua vurugu na kusababisha vifo, majeruhi, na uharibifu wa miundombinu ya Serikali na binafsi.

Taarifa hiyo ya tume imetaja sababu mbalimbali za kuongezewa muda, kwamba itasaidia kutoa fursa ya kutosha kwa kila mwenye taarifa, ushahidi au maoni, aliyepo nchini au nje ya nchi, kuwasiliana na tume ili kuhakikisha hakuna mtu au taasisi itakayokosa nafasi ya kusikilizwa.

 

 

Chanzo; Crown Media

Kuhusiana na mada hii: