Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Waandishi Wanolewa Matukio ya Ukatili

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju, amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kusimamia na kuimarisha jitihada za kuhakikisha usawa wa kijinsia unazingatiwa kama msingi muhimu wa maendeleo endelevu, ustawi wa jamii na uchumi jumuishi.

Wakili Mpanju ameyasema hayo Februari 23, 2026, jijini Arusha wakati akifungua mafunzo ya uandaaji na uwasilishaji wa habari zinazozingatia masuala ya kijinsia kwa wanahabari na wadau wa mawasiliano.

Amesema serikali inaamini kuwa maendeleo ya kweli hayawezi kupatikana ikiwa sehemu ya jamii itaachwa nje ya mchakato wa maendeleo, akisisitiza umuhimu wa kuondoa mifumo ya ubaguzi na ukosefu wa haki unaotokana na jinsia.

Aidha, ameeleza kuwa vyombo vya habari vina nafasi ya kipekee katika kuibua, kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu masuala ya usawa wa kijinsia kwa kutumia lugha inayojenga na kuunganisha badala ya kuchochea migogoro.

Amesisitiza kuwa habari zinazotolewa zinapaswa kumlenga mwananchi mmoja mmoja, zimfanye ajitambue na zimhamasishe kuwa sehemu ya suluhisho la changamoto za kijinsia.

Wakili Mpanju ameongeza kuwa serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali, wakiwemo wanahabari, asasi za kiraia na viongozi wa jamii, ili kuhakikisha elimu ya usawa wa kijinsia inawafikia wananchi katika ngazi zote.

Amesema uwezeshaji wa wanawake, vijana na makundi maalum ni nguzo muhimu katika kufikia dira ya taifa ya maendeleo shirikishi.

Kwa upande wake, Amina Mohammed kutoka mkoani Mara amesema bado kuna changamoto kubwa za ukatili wa kijinsia katika baadhi ya maeneo, hususan ukanda wa Mara, kutokana na mila na desturi zilizojengeka kwa muda mrefu.

Ameeleza kuwa elimu kwa vijana na wanawake ni silaha muhimu katika kubadili mitazamo hasi na kuwajengea uwezo wa kujitambua na kuthaminiwa katika jamii.

 

 

Chanzo; Global Publishers

Kuhusiana na mada hii: