Rais wa Chama cha wanasheria Nchini (TLS) Wakili Boniface Mwabukusi
, awajibu wanaodhani TLS ni ya wanaharakati “Activist” huku akiweka wazi nia yake juu ya dhana hiyi huku akiweka wazi ushirikiano wao na jeshi la polisi wawapo mahakamani, Sepetemba 25,2025.
“Ni yangu ni kutoa hiyo dhana nimegonga kwa unyenyekevu nafasi zote za serikali nikiwa na kusudi moja, kwenda kujitambulisha ili watu watuelewe kusudi letu ni nini, ni kiri Takukuru sikuwahi andika barua lakini tumefika karibu ofisi zote na tumezungumza wametuelewa TLS na tumekuwa na mashirikiano mazuri katika kufanya kazi”
Akaendelea kwa kusema “Sisi sio kundi la magaidi, sisi kazi yetu wakati mwendesha mashtaka anatamani mtu afungwe sisi tunambembeleza Hakimu na Jaji usimfunge mtu yawezekana sio muhalifu hilo ndio jukumu letu.”
Zaidi akasema “Mahakamani kunakuwa askari wanajua utaratibu, tunachojaribu kuwaambia wenzetu polisi kazi ya TLS tunachojitaidi ni kuleta dhana nzuri ya uwajibikaji wa pamoja.” - Mwabukusi
Pamoja na hayo Chama cha Mawakili “TLS” chini Rais wao, Wakili Boniface Mwabukusi wamewasilisha maombi yao mbele ya Jaji Mkuu pamoja IGP likiwemo kutaka mahakama kuwa na askari waliopewa mafunzo ya kimahakama imekuja baada ya kubainisha hoja kadhaa ikiwemo ya askari kuficha nyuso zao mahakamani.
“Moja ya jambo ambalo tulikuwa tukiomba na liangaliwe ni vyema mahakama ione utaratibu wa kuwa na askari wa kutosha ambao mahakama inakuwa imewafundisha kuweza kuangalia jambo hili likitokewa linafanyika namna hii ili mtu aweze kutofautisha namna ya kufanya arraignment na namna ya kushughulika na professional misconduct inayotokea mahakamani.” - Mwabukusi
Chanzo: Tanzania Journal