Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Rashid Atuhumiwa Kumua Steven kwa Wivu wa Mapenzi

Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia mwananchi mmoja kwa tuhuma za mauaji yaliyotokea wilayani Kilosa baada ya ugomvi unaodaiwa kuchochewa na wivu wa kimapenzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama, amemtaja mtuhumiwa kuwa ni Rashid Hussein Paulo (35) mkulima na mkazi wa Msowero, ambaye anatuhumiwa kumuua Steven Elia Mayungu (26) mkulima na mkazi wa Mayungu.

Tukio hilo liliripotiwa kutokea Disemba 26, 2025 majira ya saa tano usiku katika Kitongoji cha Shuleni, Kijiji na Kata ya Lumuma, Wilaya ya Kilosa, ambapo wilayani Kilosa ambapo uchunguzi wa awali umebaini marehemu alichomwa kwa kitu chenye ncha kali katika eneo la kifua baada ya kuibuka ugomvi kati yake na mtuhumiwa.

Kamanda Mkama amesema mtuhumiwa anashikiliwa kwa mahojiano zaidi na hatua za kisheria zinaendelea, huku akitoa wito kwa jamii kutatua migogoro ya kifamilia kwa njia ya amani na kufikisha masuala yao kwenye vyombo vya Dola badala ya kujichukulia Sheria mkononi.

 

 

 

 

Chanzo; Itv

Kuhusiana na mada hii: