Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia Erick Emmanuel, mkazi wa Nzuguni A, kwa tuhuma za kumuua Evance Mtui, mkazi wa Makulu Oysterbay, Jijini Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa za awali, tukio hilo lilitokea jioni ya tarehe 16 Desemba 2025, ambapo marehemu aliuawa kwa kutumia kitu chenye ncha kali.
Jeshi la Polisi limesema lilifanya msako maalum na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo, huku uchunguzi wa kina ukiendelea. Mara baada ya uchunguzi kukamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.
Jeshi la Polisi linaendelea kuwasihi wananchi kutoa ushirikiano na kuepuka vitendo vya uhalifu, huku likiahidi kuendelea kuchukua hatua kali dhidi ya wahalifu.
Chanzo; Global Publishers