Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mwanajeshi wa Marekani Akamatwa Akiwa na Mabomu Tarime

Jeshi la Polisi Kanda maalum Mkoa wa Polisi Tarime,Rorya limesema Jumapili ya November 16, 2025 saa sita mchana katika eneo la mpaka wa Tanzania na Kenya kivuko cha Sirari limemkamata Charles Onkuri Ongeta mwenye umri wa miaka 30 ambaye ana uraia pacha wa Marekani na Kenya Mwanajeshi wa Jeshi la Marekani Mwenye cheo cha Sajenti akiwa na mabomu manne aina ya CS M68 ya kurushwa kwa mkono.

Taarifa ya Polisi imeeleza kuwa wamemkamata Charles akitokea Nchini Kenya kuingia Tanzania kwa kutumia gari yenye namba za usajili KDP 502Y aina ya Toyota Landcruiser na kwamba kwa mujibu wa sheria ya umiliki wa silaha hata kama angeomba kibali cha kuingia nayo Nchini asingeruhusiwa.

"Ushahidi unaendelea kukusanywa sambamba na
kuhojiwa kwa tuhuma hizo ili hatua stahiki kwa mujibu
wa sheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake"

 

Chanzo; Wasafi

Kuhusiana na mada hii: