Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Huyu Ndiye Mwigulu Nchemba Waziri Mkuu Tanzania

Januari 7, 1975 katika Kijiji cha Makunda, Iramba mkoani Singida, alizaliwa Dk Mwigulu Lameck Nchemba, mtoto wa familia ya wakulima. Safari yake ya elimu ilianzia Shule ya Msingi Makunda, kisha Sekondari ya Ilboru na Mazengo, kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alikopata shahada ya kwanza, uzamili na PhD katika uchumi.

Kabla ya kuingia kwenye siasa, alifanya kazi katika Benki Kuu ya Tanzania kama mtaalamu wa uchumi. Mwaka 2010 alichaguliwa kuwa mbunge wa Iramba Magharibi kupitia CCM na tangu hapo ameshika nyadhifa mbalimbali za waziri wa Kilimo, Mambo ya Ndani, Sheria na Katiba, na Fedha. Novemba 13, 2025, Rais Samia Suluhu Hassan alimteua kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dk Nchemba anajulikana kwa umahiri wake katika uchumi na msimamo thabiti wa uwajibikaji. Alipokuwa Wizara ya Fedha, alisisitiza uwazi kwenye ukusanyaji mapato, matumizi ya NeST na kubadilisha kilimo kuwa biashara. Akiwa kiongozi, hajasahau mizizi yake, mara kadhaa amekuwa akisikiliza kero za wananchi Iramba.

Kupitia uteuzi wake mpya, anakabiliwa na jukumu la kuongoza serikali, kusimamia utekelezaji wa sera, kukuza uchumi na kuimarisha ajira kwa vijana. Dk Nchemba ni Waziri Mkuu wa 13 tangu Uhuru, akijumuika na viongozi waliomtangulia kama Nyerere, Kawawa, Sokoine, Pinda na Majaliwa.

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: