Dereva wa Malori Juma Maganga ambaye ni raia wa Tanzania aliyekuwa anashikiliwa Juba nchini Sudani Kusini baada ya kumgonga Mwanajeshi kitendo kilichopelekea kukamatwa na kuhukumiwa kifungo cha miaka 13 gerezani au kulipa faini amerejea nchini baaada ya kuachiwa huru Disemba 31, 2025 baada ya faini ya shilingi milioni 50 Kulipwa kutoka kwa Michango ya Wadau na Waziri wa Madini Mbunge wa Dodoma, Antony Mavunde.
Maganga amewasili Dodoma hii leo Januari 3, 2025 na kupokelewa na familia yake na amezungumza na @ayotv_ ambapo amesema kuwa alikamatwa mwezi februari mwaka jana baada ya kumgonga Mwanajeshi ambaye alipoteza maisha ambapo amewashukuru Watanzania wote waliotoa michango yao na kwa kipekee amemshukuru Mbunge Antony Mavunde kwa kumsaidia kuweza kutoka katika changamoto hiyo.
“Nawashukuru Watanzania Wote, Madereva Wote, Antony Mavunde na Serikali ya Tanzania kwa kuweza kunipambania mpaka nikaweza kutoka kwenye changamoto yangu iliyokuwa inanikabili” Amesema Juma Ally.
Chanzo; Millard Ayo