Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Bodi YavunjwaSabato kwa Tuhuma za Ubadhilifu wa Fedha

Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Rita) imeivunja Bodi ya Wadhamini ya Kanisa la Waadventista Wasabato Tanzania kufuatia tuhuma nzito za ubadhirifu wa mali na kushindwa kutekeleza majukumu kwa mujibu wa sheria. Uamuzi huo umetangazwa jijini Dar es Salaam, ukiashiria hatua kali dhidi ya tuhuma hizo.

Mtendaji Mkuu wa Rita, Frank Kanyusi, amesema hatua hiyo imechukuliwa baada ya kupokea ripoti maalumu ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), iliyobaini mapungufu makubwa katika usimamizi wa mali za kanisa.

Ukaguzi huo ulifanyika kufuatia malalamiko ya wanachama waliodai kuwepo kwa ukiukwaji wa pamoja wa wajumbe wa bodi, ikiwemo matumizi mabaya ya rasilimali za taasisi. Ripoti imeonyesha udhaifu mkubwa wa kiutawala na kisheria.

Rita imesema itawasilisha ripoti hiyo kwa vyombo vingine vya dola kwa hatua zaidi za kisheria. Wakati huohuo, kanisa limepewa siku saba kuwasilisha majina ya wajumbe 10 watakaounda kamati ya muda kusimamia shughuli hadi bodi mpya itakapoteuliwa.

Kwa upande wake, Msajili wa Jumuiya, Emmanuel Kihampa, ameonya kuwa migogoro ndani ya taasisi za kidini isipotatuliwa mapema huweza kusababisha mpasuko, mgawanyiko na kuvuruga amani ya taasisi pamoja na jamii kwa ujumla.

 

 

Chanzo; Mwananchi Scoop

Kuhusiana na mada hii: