Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Afisa DAWASA Aliyepokea Rushwa Abanwa Mahakamani

Mtumishi wa DAWASA Kibamba, amehukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Ubungo, kulipa faini ya kiasi cha Shilingi 1,000,000 na kurejesha fedha kiasi cha Shilingi 297,000 ambazo alizipokea kutoka kwa mlalamikaji, ikiwa ni fedha za rushwa ili arejeshe huduma ya maji aliyokuwa ameisitisha kwa kosa la kujiunganishia kinyume na taratibu (by pass).

Katika shauri hilo Na. 15649/2025, Mshtakiwa Nsajigwa Dominico Mwaipyana ambaye ni Afisa Msaidizi DAWASA Kibamba, alishtakiwa kwa makosa mawili ya kuomba rushwa ya kiasi cha Shilingi 300,000 na kupokea kiasi cha Shilingi 297,000 kinyume na kifungu cha 15(1) (a), 2 na 3(b) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa SURA 329 R.E 2022, kutoka kwa mteja aliyesitishiwa huduma baada ya kujiunganishia maji hayo kinyume na taratibu.

Mshtakiwa alipatikana na hatia kwa makosa yote mawili na kuhukumiwa kilipa faini ya Shilingi 500,000 kwa kila kosa au kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela na kurejesha fedha kiasi cha Shilingi 297,000 alizopokea.

Shauri hilo liliendeshwa na wanasheria Khanifa Kapinga na Sophia Nyanda.

 

 

 

Chanzo; Itv

Kuhusiana na mada hii: