Spika wa Bunge, Mussa Zungu ameitaka Wizara ya Maji kufuatilia sababu za kuendelea kutolewa bili za maji kwa wakazi wa Dar es Salaam licha ya kuwapo kwa uhaba mkubwa wa maji kwa kipindi kirefu.
Akizungumza leo Jumatano, Januari 28, 2026, bungeni jijini Dodoma, Zungu amesema hali hiyo ni kero kwa wananchi na inahitaji hatua za haraka.
“Kulikuwa na uhaba mkubwa sana wa maji Dar es Salaam lakini bili zinaendelea kuja kama kawaida. Shida ni nini? Kalifanyie kazi,” amehoji Zungu.
Chanzo; Mwananchi