Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamshikilia mkazi wa kijiji cha Madundasi kilichopo wilayani Mbarali, Doto Lubongeja kwa tuhuma za mauaji ya watoto watatu wa familia moja kwa kuwanyonga na kamba shingoni.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya,Wilbert Siwa, amewataja watoto waliouawa ni Petro Amosi(8), Samu Amosi(6) na Nkamba Amosi(4) wote wakazi wa Kijiji cha Madundasi.
Amesema tukio hilo lilitokea jana Januari 15, 2026 kijijini hapo, ambapo mtuhumiwa aliua watoto hao baada ya kuwakuta peke yao wakichunga ng’ombe jirani na nyumbani kwao.
Amesema baada ya kutekeleza mauaji hayo aliiba ng’ombe 15 kisha kuziswaga na kuzificha nyumbani kwa mjomba wake aitwaye Masoda Kulwa, anayeishi Kijiji cha Madundasi B na kuanza kutafuta mteja, ambapo aliuza ng’ombe hao na kupata fedha Sh milioni 5.1
-
Ambapo amesema kufuatia tukio hilo, pilisi walianza msako mkali na kufanikiwa kumkamata Doto Lubongeja pamoja na Masoda Kulwa, ambaye walishirikiana kuuza ng’ombe hao.
Chanzo; Eatv