Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Aliyetoroka Gerezani Akamatwa Tena

Katika kipindi cha mwezi mmoja, Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limewatia hatiani watuhumiwa 55 kwa makosa mbalimbali, ikiwemo unyang’anyi wa kutumia silaha ambapo watuhumiwa 9 walihusiana na tukio hilo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi, amesema tangu Januari 1, mwaka huu, jeshi limefanikiwa kwa kiwango kikubwa kupambana na uhalifu kwa kulinda usalama wa raia na mali zao.

Miongoni mwa watuhumiwa wa unyang’anyi ni Alli Ramadhani maarufu kama (Bwengo), mwenye umri wa miaka 36, mkazi wa Amboni jijini Tanga, ambaye alikamatwa Agosti 19, 2025 akiwa na makosa mengine. Aliwahi kuhudumia kifungo cha miaka 30 jela lakini alitoroka kutoka Gereza la Maweni, jijini Tanga.

Kamanda Mchunguzi ameendelea kutoa wito kwa wananchi kushirikiana na jeshi la polisi kuwabaini wahalifu na kuchukua hatua stahiki za kisheria dhidi yao.

 

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: