Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Waliopora Milioni 54 na Kujeruhi, Mmoja Ashikwa

Jeshi la polisi mkoani Songwe, linamshikilia mtu mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa kwa ajili ya upelelezi, kwa tuhuma za kuhusika na tukio la unyang’anyi wa kutumia silaha aina ya Bunduki, ambapo akiwa na wenzake alimjeruhi maeneo ya kiuno Bw. Yengo Mwapina mkazi wa eneo la Sogea, alipokuwa akitoka benki , tukio ambalo limetokea Februari 04 mwaka huu majira ya asubuhi, katika eneo la Kisimani Kata ya Tunduma wilayani Momba mkoani humo.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe SACP Augustino Senga, amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa katika moja ya mkoa jirani, baada ya kupata taarifa fiche za kiitelejensia, ambapo wanaendelea kuwasaka watuhumiwa wengine waliohusuka na tukio hilo, huku akitoa onyo kali kwa watu wote wanaojihususha na matukio ya ujambazi .

 

 

 

Chanzo; Itv

Kuhusiana na mada hii: