Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameweka wazi kusitishwa kwa usafiri wa mabasi yaendayo haraka maarufu mwendokasi kwa ajili ya tathimini ya kile kilichofanyika tarehe 29,2025.
Ameweka wazi hayo akizungumza na waandishi wa habari Novemba 4, 2025, Jijini Dar es Salaam
“Vituo vya mwendokasi vimeharibiwa kwa mantiki hiyo tunaendelea kuusitisha usafiri huo huu kwa njia ya Morogoro na Mbagala.” Amesema Chalamala
Huku akiendelea kwa kusema “ Usafiri huu umekuwa ukiwasaidia wengi tunausitisha mara moja ili kufanya tathimini ya kina uharibifu uliotokea.”
Zaidi, Albert Chalamaila avitaka vituo vya mafuta kufunguliwa pamoja nakuonya utatratibu unaotumika kuuzia mafuta.